1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LAGOS : Gavana wa Nigeria mbaroni Uingereza

17 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEaQ

Polisi wa masuala ya udanganyifu mjini London wamemkamata gavana wa Nigeria na mtetezi wa kikabila na kuchochea tishio la wanamgambo kuwashambulia raia wa Uingereza na mitambo yake ya mafuta katika jimbo tete la Delta nchini Nigeria.

Gavana Diepreye Alamieyeseigha wa jimbo lenye utajiri wa mafuta la kusini nchini Nigeria la Bayelsa alikamatwa Alhamisi mjini London na kuachiliwa baadae kwa dhamana huku uchunguzi ukiendelea.

Msemaji wa Tume ya Uhalifu wa Kiuchumi na Fedha nchini Nigeria Osita Nwajaj amesema kukamatwa kwa gavana huyo kunahusiana na madai ya uchunguzi wa fedha zilizopatikana kwa njia isio halali unaofanywa na polisi wa jiji kuu la Uingereza.

Kwa mujibu wa repoti tano za magazeti ya Nigeria zinazofanana wapelelezi wa shirika la Scotland Yard la Uingereza wamegunduwa pauni milioni moja sawa na dola milioni moja na laki nane ikiwa ni fedha taslimu katika nyumba ya gavana huyo mjini London.