1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kwanini Wapakistan wanaliunga mkono kundi la Taliban?

21 Julai 2021

Raia wengi wa Pakistan wamekuwa wakiwaunga mkono wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan, wakati ambapo vikosi vya kigeni vikiwemo vile vya Marekani vikiondoka nchini humo.

https://p.dw.com/p/3xmkR
Afghanistan Taliban Waffenstillstand
Picha: JAVED TANVEER/AFP/Getty Images

Hali hiyo imeashiria ushawishi wa kundi hilo miongoni mwa raia wa Pakistan na Afghanistan. Siku za hivi karibuni nchi hizo mbili zilitupiana lawama kuhusu swala la kuwaunga mkono wapiganaji wa Taliban.

Mfano mmoja wapo ni kijana Abdul Rasheed raia wa Pakistan aliyefariki kwenye jimbo la Ngangarhar nchini Afghanistan mapema mwezi huu. Mamia ya watu waliohudhuria mazishi ya kijana huyo wa miaka 22 karibu na Peshawar walisikika wakiimba nyimbo zinazounga mkono kundi la Taliban.

Kwenye mitandao ya kijamii, picha za vidio za raia wa Pakistan waliobeba bendera za Taliban na kuimba nyimbo za kundi hilo zilizagaa mitandaoni. Hayo yametokea wakati ambapo wapiganaji wa Taliban wanaendelea kuyadhibiti maeneo kadhaa ya Afghanistan huku vikosi vya mwisho vya Marekani na washirika wake vikiwa vinakaribia mwisho wa uwepo wake nchini humo.

Wahubiri wa kiislamu kwenye maeneo kadhaa ya Pakistan wamekuwa wakiwahimiza raia kuwaunga mkono Wataliban na kutoa miito ya kupatikana misaada.

Pakistan Grenzstadt Chaman Menschen mit Taliban-Flagge
Wapakistan wakipeperusha bendera za TalibanPicha: Asghar Achakzai/AFP/Getty Images

Wakaazi wengi kwenye mji wa Quetta na mkoa wa Pishin, jimboni Balochistan, wameimbia DW kwamaba kuna ongezeko la watu wanaowaunga mkono Wataliban.

Hata hivyo mkazi mmoja amesema ijapokuwa Wataliban wanaungwa mkono kwenye eneo lao, maandamano ya kuwapinga hayawezi kufanikiwa bila kuungwa mkono wa viongozi wa serikali. Amesema mwanzoni wahubiri walikuwa wakiomba michango misikitini kwa ajili ya Taliban, lakini hivi sasa wanaenda nyumba hadi nyumba kuomba michango ambayo wansdma ni kwa ajili ya wa vita vitakatifu vya afhanistan.Mapambano na Taliban yashika kasi Afghanistan

Lakini maafisa wa Pakistan wamesema taarifa hizo za maandamano ya kuwaunga mkono na misaada kwa Wataliban ni za uzushi. Zahid Hafeez Chaudhary, msemaji wa wiraza ya mambo ya nje ya Pakistan ameimabia DW kuwa madai hayo hayana msingi wowote na hayatokei nchini humo.

 Kundi la Tehrik-i-Taliban Pakistan (TTP) limepigwa marufuku nchini Pakistan ,lakini  wataalamu wanasema tuhuma za kwamba serikali inaliunga mkono unalipa nguvu kundi hilo.

Pakistan Islamabad | Imran Khan, Premierminister
Waziri Mkuu wa Pakistan Imran KhanPicha: Saiyna Bashir/REUTERS

 Wanamgambo wa Taliban wameyadhiti maeneo kadhaa nchini Afghanistan katika siku za hivi karibuni. Na wamekuwa wakiwahimiza raia wa Pakistan kujiunga nao nchini Afghanistan. makumi ya Wapakistan waliuliwa kwenye uwanja wa mapambano miezi ya hivi karibuni wakiwaunga mkono Wataliban dhidi ya vikosi vya serikali.

 Wachambuzi wamesema viongozi wa Pakistan hawajachukuwa hatua yeyote kuzuwiya raia wake kujiunga na Wataliban kwenye nchi jirani ya Afghanistan. Mitandao ya kijaami imekuwa ikionyeshaa picha za mazishi ya wapiganaji waliouliwa nchini Afhganistan. mamia ya watu walihudhuria mazishi ya wapiganaji wa pakistani ambao mili yao ilirejeshwa makwao.

 Michael Kugelman, naibu mkuu wa taasisi ya Wilson Center kuhusu Asia kusini amesema ungwaji mkono wa Pakistan sio tu kuigeuza ardhi yake kuwa maficho kwa viongozi wa kundi la Taliban bali pia huduma za kiafya kwa kundi hilo na kwa familia za wapiganaji wake.

Kugelman amesema msimamo wa Pakistan wa hapo awali wa kupatanisha kundi la Taliban na Marekani na baadae taliban na  serikali ya Afghjanistan , umetofautiana na madai kwamba haina ushawishi wa kutosha dhidi ya Wataliban.

Amesema kunauungwaji mkono mkubwa wa Wataliban ncchini Pakistan, na kwa miaka kadhaa raia wa Pakistan wamejiunga na kundi la taliban akama wapiganaji.

Vita vya maneno viliongezeka mwezi huu kati ya Afghanistan na Pakistan baada ya Makamu wa Rais wa Afghanistan kulituhumu jeshi la Pakistan kwa kutoa msaada wa angani kwa Taliban katika maeneo fulani. Pakistan ilikanusha vikali madai hayo.