1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kwanini Qatar ni mpatanishi bora kuliko Mataifa mengine?

21 Agosti 2024

Wakati mazungumzo yanayolenga kusitisha mapigano Gaza yakiendelea, wapatanishi wa Qatar wako katika harakati nyengine kujaribu kutatua mizozo mingine duniani. Je kipi kinachoifanya kuwa msuluhishi mzuri katika mizozo?

https://p.dw.com/p/4jkQI
Qatar | Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al Thani
Waziri Mkuu wa Qatar ambaye pia ni Waziri wa mambo ya nje wa taifa hilo Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al Thani Picha: Murat Gok/Anadolu/picture alliance

Maafisa kutoka Urusi na Ukraine hawajakutana angu walipofanya hivyo muda mfupi baada ya vita kati yao kuanza mwaka 2022, wakati wanajeshi wa Moscow walipoivamia Kiev. Lakini hivi karibuni taarifa zilienea kwamba kuna uwezekano wa kufanyika mazungumzo, ya kuwapatanisha majirani hao wawili yatakayosimamiwa na Qatar. Kwa bahati mbaya mazungumzo hayo yalifutwa kufuatia hatua ya Ukraine kujibu mashambulizi ya Urusi kwa kulivamia eneo la Kursk. Hata hivyo taarifa za uwezekano wa mazungumzo hayo kufanyika ni ushindi kwa Qatar nchi ndogo tajiri kwa gesi, iliyoko katika Guba ya kiarabu.

Mazungumzo ya usuluhishi mzozo wa Gaza yaingia siku ya pili

Hii sio mara ya kwanza Qatar imejihusisha na mizozo nje ya Mashariki ya kati. Imewahi kusaidia katika mipango ya kuwaachia wamarekani walioshikiliwa Iran, Afghanistan na Venezuela, pamoja na kuwarejesha watoto wa Ukraine kwa familia zao, baada ya kuchukuliwa na kupelekwa Urusi. Qatar pia imesimamia juhudi za kidiplomasia za kufikiwa amani kati ya Sudan na  Chad, Eritrea na Djibouti pamoja na kuhusika na makubaliano ya amani ya Darfur ya mwaka 2011.

Mwaka 2020  Qatar ilishiriki katika mchakato wa kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani nchini Afgnanistan kwa kuzungumza na watawala wa Taliban na mwezi Novemba mwaka 2023, wapatanishi wa Qatar walisaidia kupatikana usitishwaji mapigano kwa muda katika mzozo wa Gaza.

Qatar mpatanishi wa dunia

Burcu Ozcelik, mtafiti mkuu katika taasisi ya utafiti wa sera ya Royal United Services Institute ya Uingereza ameiambia DW kwamba, Qatar kuibuka kuwa mpatanishi mkuu imeinua hadhi yake kidiplomasia na kuipa sura mpya kutoka kuwa msuluhishi wa kikanda hadi kuwa mhusika muhimu katika jukwaa la dunia na jukumu hilo jipya linaongeza ushawishi wa Qatar kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwa mshirika mzuri wa amani duniani.

Israel yaendelea kukabiliana na Hezbollah

Mzozo wa Mashariki ya Kati
Mwezi Novemba mwaka 2023, wapatanishi wa Qatar walisaidia kupatikana usitishwaji mapigano kwa muda katika mzozo wa Gaza.Picha: Saudi Press Agency/APA/ZUMA/picture alliance

Wachambuzi wanasema Qatar imejiweka katika nafasi hiyo kwa lengo la kujiimarisha kiusalama katika kanda isiyokuwa tulivu. Awali mtafiti mmoja kwa jina Ali Abo Rezeg, aliwahi kuelezea katika jarida moja la mwaka 2021 kwamba, Qatar inajiingiza katika uwanja huo wa diplomasia kwa kutaka kushindana na wapinzani wake kama Umoja wa Falme za Kiarabu  na kukataa pia kushurutishwa na nchi kubwa zaidi ambaye ni jirani yake Saudi Arabia.

Kwanini Waqatari ni wazuri kwa masuala ya upatanishi?

Mahusiano ni muhimu na Qatar inajulikana kwa mtandao wake mpana wa mawasiliano, imeunga mkono makundi mengi tofauti kwa kuwapa hifadhi, ufadhili au silaha. Makundi haya yanajumuisha kundi la Taliban, udugu wa kiislamu au Muslim Brotherhood nchini Misri, wanamgambo wa Libya na wanapinduzi wa Syria, Tunisia na Yemen wakati wa vuguvugu la mataifa ya Kiarabu.

Qatar yaendeleza juhudi za upatanishi kati ya Israel na Hamas

Vile vile Qatar iliipa Marekani nafasi ya kuweka kambi yake ya kijeshi nchini humo ya Al Udeid tangu mwaka 2001 na sasa imekuwa moja ya kambi kubwa zaidi za kijeshi katika eneo la Mashariki ya kati iliyo na wanajeshi 10,000. Mwaka 2022 rais wa Marekani Joe Biden aliitaja  Qatar kama mshirika wa NATO kufuatia jukumu lake katika mazungumzo ya Aghanistan na kuwaondoa wanajeshi wa Marekani.

Israel yazidisha mashambulizi katika ukanda wa Gaza

Hata hivyo kuwa "mpatanishi wa ulimwengu" kunaweza pia kukuweka katika nafasi ngumu. Katika mazungumzo ya sasa  kati ya Israel na Hamas wachambuzi wanasema Qatar imejikuta katika wakati mgumu. Israel imeishutumu kuwa na sura mbili upatanishi huku ikifadhili ugaidi.

Nao wanasiasa wa Marekani wametoa wito wa uhusiano wa Marekani na Qatar kuangaliwa upya iwapo nchi hiyo haitotoa shinikizo kwa Hamas. Mwezi Aprili wanasiasa wengine  wa Marekani waliwasilisha muswada ambao ungeweza kuiondoa Qatar kama mshirika muhimu wa NATO. Qatar imekanusha  madai yote ikisema haina usemi juu ya Hamas.