Barani Afrika kuliwahi kuwa na marais wanawamke , lakini sasa hakuna. Kwingineko pia waliowahi kuwa marais wanawake baadhi yao wameondolewa madarakani. Hali inaonyesha kuwa uwakilishi wao katika ngazi za maamuzi kama wakuu wa nchi unazidi kupungua. Je hali hiyo inasababishwa na nini? Ni swali ambalo Yusra Abdallah Buwayhid analiuliza na akina mama wanatoa majibu.