1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kutambua mzozo wa hali ya hewa kama dharura ya kiafya

26 Oktoba 2023

Wanasayansi kote ulimwenguni wamelitolea mwito Shirika la afya ulimwenguni, WHO kutangaza mzozo wa hali ya hewa na upotevu wa bayoanuwai kuwa ni dharura ya kiafya.

https://p.dw.com/p/4Y2cT
Wataalamu wataka hatua za kutambua mzozo wa hali ya hewa kama dharura ya kiafya
Wataalamu wataka hatua za kutambua mzozo wa hali ya hewa kama dharura ya kiafyaPicha: Pond5 Images/IMAGO

Zaidi ya majarida 200 ya kisanyansi jana Jumatano yamechapisha onyo juu ya kitisho kilichopo, ili kujiandaa kabla ya Mkutano wa kimataifa wa Afya katika majira ya machipuko ya 2024. Miongoni mwa majarida hayo ni The Lancet na The British Medical Journal (BMJ).

Mhariri mkuu wa jarida la BMJ Kamran Abbasi amesema ni hatari kutofautisha majanga hayo kwa kuwa vyote huathiri afya za binadamu na vina mahusiano.  

Mabadiliko ya hali ya hewa yamechangia kusambaa kwa magonjwa ya kuambukiza, uchafuzi wa mazingira unaoharibu vyanzo maji ya kunywa na upungufu wa samaki unaosababishwa na uchafuzi wa bahari.