1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura zahisabiwa Jamhuri ya Afrika ya Kati

31 Julai 2023

Shughuli ya kuhesabu kura inaendelea katika Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya kupigwa kura ya maoni kuhusu katiba mpya, ambayo inalenga kumruhusu Rais Faustin Archange Touadera kugombea kwa muhula wa tatu.

https://p.dw.com/p/4UaEh
Zentralafrikanische Republik Präsident austin-Archange Touadera
Picha: Antoine Rolland/REUTERS

Karibu raia milioni 1.9 walisajiliwa kushiriki kura ya mapendekezo ya mabadiliko hayo yatakayoongeza mamlaka ya rais kutoka muhula wa miaka mitano hadi saba na kuondoa ukomo wa mihula miwili.

Mwaka 2020, Touadera alishinda muhula wa pili hadi mwaka 2025, baada ya uchaguzi kuvurugwa na baadhi ya makundi ya waasi, lakini pia uliokabiliwa na madai ya udanganyifu.

Wapinzani wake sasa wanamshutumu kwamba anataka kuwa rais wa maisha.

Matokeo ya mwanzo yanatarajiwa kutolewa baada ya siku nane.

Mahakama ya katiba inatarajiwa kuchapisha matokeo rasmi Agosti 27.