1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura zaanza kuhesabiwa Rwanda baada ya uchaguzi mkuu

15 Julai 2024

Zoezi la kuhesabu kura katika uchaguzi wa rais na bunge nchini Rwanda limeanza jioni hii.

https://p.dw.com/p/4iIXy
Uchaguzi wa Rwanda 2024 l Mpigakura, Kigali
Raia wa Rwanda akipiga kura katika uchaguzi mkuu wa Julai 15, 2024.Picha: Guillem Sartorio/AFP via Getty Images

Hiyo ni baada ya kufanyika uchaguzi ambao rais wa sasa Paul Kagame akitarajiwa kwa kiasi kikubwa kupata ushindi na kuendelea kubakia madarakani kwa muhula mwingine wa miaka mitano.Wafahamu wagombea wawili wanaochuana na Kagame

Kagame anayeiongoza Rwanda tangu yalipomalizika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 na aliyechaguliwa kuwa rais mwaka 2000, anakabiliana na wapinzani wawili kwenye uchaguzi huo,Frank Habineza anayekiongoza chama cha Kijani na mgombea huru Phillipe Mpayimana. 

Wakosoaji wake wengi wenye umaarufu walizuiwa kugombea kwenye uchaguzi huo.Zaidi ya wanyarwanda milioni tisa waliandikishwa kupiga kura katika vituo 2,433 vilivyowekwa nchi nzima. Shughuli ya kuhesabu kura ilipangwa kuanza mara moja baada ya vituo vya kupiga kura kufungwa alasiri kwa saa za Rwanda.Paul Kagame kusalia madarakani hadi mwaka 2034?

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW