1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura ya maoni yaonesha Putin anaweza kushinda asilimia 82

12 Machi 2024

Uchunguzi mpya wa maoni unaonesha Rais wa Urusi Vladimir Putin anaweza kushinda hadi asilimia 82 ya kura katika uchaguzi ujao wa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4dPSM
Russland | Putin hält Rede zur Lage der Nation
Putin akitoa hotuba yake ya kila mwaka kwa Bunge la Shirikisho, mjini Moscow, Urusi, Februari 29, 2024.Picha: Evgenia Novozhenina/REUTERS

Matokeo hayo ni kwa mujibu wa uchunguzi wa wapiga kura wanaostahiki uliofanywa na taasisi ya utafiti wa maoni ya VCIOM yenye kuegemea upande wa mamlaka.

Wagombea watatu wa upinzani, ambao wanamuunga mkono waziwazi Putin au wanaofuata mwelekeo wa serikali ya Kremlin, wanaonekana kuwa na uwezo wa kupata asilimia 5 na hadi 6 kila mmoja.

Kura za maoni za Urusi zinatazamwa kama mbinu muhimu ya serikali kufanya tathmini ya ufanisi wa propaganda za Kremlin, kwa zingatio la vyombo vya  habari vya umma. Televisheni ya serikali inayodhibitiwa na Kremlin, inatazamwa zaidi na wazee wa Kirusi katika maeneo ya vijijini, wanamwonyesha Putin kama mtu asiyekuwa na mbadala.