1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Kundi la JNIM ladai kuishambulia kambi ya jeshi Mali

Sylvia Mwehozi
9 Septemba 2023

Kundi linalofungamana na Al-Qaeda la Jamaatu Nusra al-Islam wal-Muslimin, JNIM, limedai kuhusika na shambulio la kujitoa mhanga katika kambi ya kijeshi kaskazini mashariki mwa Mali jana Ijumaa.

https://p.dw.com/p/4W8Zc
Mali Unruhen Soldaten
Picha: Sebastien Rieussec/Hans Lucas/IMAGO

Kundi linalofungamana na Al-Qaeda la Jamaatu Nusra al-Islam wal-Muslimin, JNIM, limedai kuhusika na shambulio la kujitoa mhanga katika kambi ya kijeshi kaskazini mashariki mwa Mali jana Ijumaa.

Shambulio hilo lilitokea siku moja baada ya mamlaka nchini humo, kulituhumu kundi hilo kwa kufanya mashambulizi mawili kwenye kambi nyingine ya kijeshi na boti yaliyoua zaidi ya watu 60.

Kuongezeka kwa ukosefu wa usalama kumechochea mapinduzi ya kijeshi katika nchi tatu zilizoathirika zaidi na uasi za Mali, Burkina Faso na Niger.

Mali ni mojawapo ya nchi kadhaa za Afrika Magharibi zinazopambana na uasi wa vurugu unaohusishwa na makundi ya al Qaeda na lile linalojiita Dola la Kiislamu IS.