1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KUALA LUMPUR: Jeshi la kiislamu kupelekwa kusini mwa Lebanon

3 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDPH

Muungano wa mataifa ya kiislamu unatafakari juu ya kuundwa kwa jeshi la waislamu litakalolinda amani kusini mwa Lebanon. Muungano huo unataka pia Israel ichunguzwe kwa uhalifu wa kivita.

Wajumbe wa mkutano wa dharura wa muungano wa mataifa ya kiislamu uliofanyika mjini Kuala Lumpur nchini Malaysia, wametoa taarifa ya pamoja inayotaka jeshi la kiislamu lichukue jukumu la kulinda amani kusini mwa Lebanon chini ya mamlaka ya Umoja wa Mataifa.

Taarifa hiyo inataka pia Israel ichunguzwe kwa uhalifu wa kivita katika kampeni yake ya kuyavamia maeneo ya Lebanon na Gaza. Watu takriban 643 wameuwawa nchini Lebanon, wengi wao wakiwa ni raia. Waisraeli 56 wameuwawa katika vita hivyo.