1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kremlin yasema Putin yupo imara

27 Juni 2023

Ikulu ya Kremlin leo imepuuza maoni yanayotolewa na wachambuzi kadhaa wa siasa duniani kwamba uasi uliofanywa na kundi la mamluki la Wagner umetikisa nafasi ya Rais Vladmiri Putin kama kiongozi mwenye nguvu nchini Urusi.

https://p.dw.com/p/4T8Ka
Russland l russische Präsident Putin spricht auf dem Kathedralenplatz am Kreml
Picha: Sputnik/Sergei Guneev/Pool via REUTERS

Msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov, amesema uasi huo uliozimwa badala yake umeonesha jinsi jamii ya Kirusi ilivyoshikamana na rais Putin hata katika nyakati za mashaka. 

Wakati huo huo, Rais Putin amewahutubia wanajeshi wa nchi yake na kuwasifu kwa kuzuia kile alichosema ni "vita vya wenyewe kwa wenyewe" ambavyo vingetokea kutokana na uasi wa kundi la Wagner. 

Kwenye hotuba yake, Putin pia amekiri kwa mara ya kwanza kwamba Moscow imekuwa ikilipatia fedha kundi la Wagner licha ya hapo kabla Urusi kukanusha kuwa haina mafungamano la kundi hilo.