1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kremlin: Ripoti ya Washington post kuhusu Ukraine yashtusha

13 Novemba 2023

Ikulu ya Urusi imesema ripoti iliyochapishwa na gazeti la Washington Post la Marekani kuwa afisa wa kijeshi wa Ukraine aliratibu mashambulizi kwenye mabomba ya Nord Stream ya Urusi ni ya kushtusha

https://p.dw.com/p/4Yl13
Rais wa Ukraine Vladimir Zelensky
Rais wa Ukraine Vladimir ZelenskyPicha: president.gov.ua

Washington Post iliripoti kwamba afisa huyo mwandamizi wa kijeshi wa Ukraine Roman Chervinsky alipokea maagizo kutoka maafisa wa ngazi za juu wa Ukraine ambao huripoti kwa Mkuu wa Jeshi Jenerali Valery Zaluzhnyi.

Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amesema taarifa za Ukraine kuhusika na hujuma hizo za kigaidi zinazidi kuongezeka katika ripoti na uchunguzi wa vyombo vya habari.

Urusi yahamishia baadhi ya wanajeshi wake Mashariki mwa Ukraine

Amesema hiyo ni dalili ya kutia wasiwasi sio tu kwa upande wao, bali pia kwa mataifa ya magharibi.