1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin yuko tayari kuzungumza na kansela Scholz wa Ujerumani

26 Mei 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema yuko tayari kwa duru mpya ya mazungumzo ya simu na kansela wa Ujerumani Olaf Scholz kuhusiana na vita nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4Rs1U
Russland | Dmitri Peskow
Picha: Sergei Savostyanov/TASS/dpa/picture alliance

Msemaji wa Putin Dmitry Peskov amesema kiongozi huyo bado yuko tayari kwa mazungumzo, ingawa amesisitiza bila shaka atazingatia lengo lake la msingi la kulinda maslahi ya watu wake.

"Scholz bado hajampigia Putin, na sina taarifa yoyote iwapo Ujerumani imeratibu mazungumzo kwa njia ya simu. Bila shaka ni muhimu kuzungumza. Rais Putin yuko tayari kwa mazungumzo. Na wakati huohuo, akizingatia lengo kuu la kulinda maslahi ya taifa letu," alisema Peskov.

Kulingana na ikulu ya Kremlin, Putin na Scholz kwa mara ya mwisho walizungumza kwa simu Disemba 2, 2022 yaliyodumu kwa karibu saa moja. Mazungumzo hayo yaliyoratibiwa na Ujerumani yaliangazia mzozo wa na matokeo ya vita.