1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin kukutana na Erdogan siku ya Jumatatu mjini Sochi

Sylvia Mwehozi
1 Septemba 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin anatarajiwa kukutana na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Urusi ya Kremlin.

https://p.dw.com/p/4Vr8y
Erdogan und Putin (Archivbild)
Picha: Sputnik/Xinhua/IMAGO

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amewaeleza waandishi wa habari kwamba mazungumzo ya viongozi hao wawili yatafanyika katika mji wa Sochi.

Mkutano huo utafanyika huku kukiwa na matumaini kwamba Putin na Erodan wataweza kufufua makubaliano ya usafirishaji salama wa nafaka za Ukraine.

Tangazo la Moscow limetolewa muda mchache baada ya Ukraine kudai kwamba meli mbili zaidi, zimeanza safari kupitia njia ya muda iliyoanzishwa na Kyiv ili kuhakikisha usafirishaji salama.

Urusi ilijiondoa katika makubaliano hayo yanayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na Uturuki na kuonya kuwa meli zinazoondoka katika bandari za Ukraine zinaweza kulengwa kwa mashambulizi ya kijeshi.