1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korti ya Sudan yaagiza kurudishwa kwa huduma za Intaneti

10 Novemba 2021

Mahakama ya Sudan imepitisha uamuzi unaotaka huduma za mtandao wa Intaneti zilizokatwa wakati wa mapinduzi ya kijeshi zaidi ya wiki mbili zilizopita kurudishwa.

https://p.dw.com/p/42oRo
Sudan Armee
Picha: Getty Images/AFP/E. Hamid

Hata hivyo, licha ya uamuzi huo wa mahakama huduma za mtandao bado zilikuwa zimezimwa mapema leo.

Wakili Abdelazim Hakim ameliambia shirika la habari la AFP kuwa mahakama ya mjini Khartoum imeagiza huduma za Intaneti kurudishwa mara moja.

Kesi hiyo ilikuwa imewasilishwa na kundi la wanasheria na chama cha kulinda maslahi ya wateja wa Sudan waliopinga kuzimwa kwa mtandao.

Mtandao wa Intaneti ulikuwa umezimwa kote nchini Sudan tangu Oktoba 25, wakati jeshi lilipofanya mapinduzi na kuiondoa madarakani serikali ya mpito na pia mawasiliano ya simu yalikatizwa wakati huo.

Jenerali Mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan aliivunja serikali na kutangaza hali ya hatari kando na kuwakamata baadhi ya viongozi wa kiraia.