1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korti kusikiliza kesi ya Trump ya kinga ya kushtakiwa Aprili

29 Februari 2024

Mahakama ya juu ya Marekani imekubali kusikiliza madai ya Donald Trump kwamba kama rais wa zamani, ana kinga ya kushtakiwa.

https://p.dw.com/p/4d0E0
USA Columbia | Donald Trump baada ya kura ya awali South Carolina
Rais wa zamani wa Marekani, Donald TrumpPicha: Andrew Harnik/AP Photo/picture alliance

Hatua hiyo inachelewesha zaidi kesi dhidi yake kuhusu njama ya kutaka kupindua matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.

Mahakama hiyo ya juu zaidi Marekani imesema itasikiliza kesi hiyo katika wiki ya Aprili 22 na kuongeza kuwa, kesi hiyo ya kutaka kupindua matokeo ya uchaguzi, itasimama kwa sasa.

Marekani | Mahakama ya Juu ya Marekani Washington | Maandamano
Bango la kupinga Trump kushiriki uchaguzi wa rais mbele ya Mahakama ya Juu ya MarekaniPicha: Manuel Balce Ceneta/AP Photo/picture alliance

Trump ameupokea vyema uamuzi huo wa mahakama ya juu akisema, bila kinga ya kushtakiwa, rais hawezi kutimiza majukumu yake kikamilifu na kufanya maamuzi kwa ajili ya Marekani.

Trump alikuwa ameratibiwa kufunguliwa mashtaka Machi 4 kwa njama ya kupindua matokeo ya uchaguzi ulioshindwa na Rais Joe Biden.

Majaji watatu wa mahakama ya rufaa mapema mwezi huu wa Februari, waliamua kwamba Trump mwenye umri wa miaka 77, hana kinga ya kushtakiwa kama rais wa zamani.

Hakuna rais mwengine yeyote wa Marekani aliyekuwa amefunguliwa mashtaka mahakamani, kabla Donald Trump.