1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiKorea Kusini

Korea yapiga marufuku ulaji na biashara ya nyama ya mbwa

9 Januari 2024

Hatua rasmi ya kuunga mkono kupigwa marufuku utamaduni huo, imepata umaarufu zaidi chini ya Rais Yoon Suk Yeol ambaye binafsi ni mpenzi wa wanyama.

https://p.dw.com/p/4b1Dq
Marufuku ya ulaji wa nyama ya mwa Korea Kusini
Marufuku ya ulaji wa nyama ya mwa Korea KusiniPicha: Mohammad Taufan/AP Photo/picture alliance

Sheria hiyo itaanza kutekelezwa mwaka 2027. Katika nchi hiyo, ulaji nyama ya mbwa ni jambo la kawaida ambalo wanaharakati kwa muda mrefu wamekuwa wakikiita ni kitendo kinachoifedhehesha Korea Kusini kimataifa.

Hatua rasmi ya kuunga mkono kupigwa marufuku utamaduni huo, imepata umaarufu zaidi chini ya Rais Yoon Suk Yeol ambaye binafsi ni mpenzi wa wanyama na mkewe ni mkosoaji mkubwa wa biashara ya nyama ya mbwa.

Inaaminika kwamba wakati mmoja zaidi ya mbwa milioni moja walichinjwa kwa mwaka kwa ajili ya kitoweo.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW