1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kusini yamwita balozi wa Urusi

21 Juni 2024

Korea Kusini imemwita balozi wa Urusi kupinga mkataba wa ushirikiano wa kijeshi kati ya Korea Kaskazini na Urusi uliosainiwa kwenye ziara ya Rais Vladimir Putin mjini Pyongyang mapema wiki hii.

https://p.dw.com/p/4hLxi
Putin kwa Kim Jong Un
Rais Vladimir Putin wa Urusi (kushoto) akiwa na mwenyeji wake, Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jung Un.Picha: GAVRIIL GRIGOROV/AFP/Getty Images

Balozi Georgy Zinoviev anayeiwakilisha Moscow ameitwa na serikali ya Korea Kusini kwa ajili ya kutoa maelezo ikiwa ni sehemuj ya hatua ya Seoul kupingana na makubaliano kati ya Urusi na Pyongyang.

Serikali mjini Seoul imeitaka Urusi kuacha mara moja ushirikiano wa kijeshi na Korea Kaskazini na kuheshimu maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. 

Soma zaidi: Putin kusaini mikataba ya ushirikiano wakati wa ziara mjini Pyongyang

Korea Kaskazini imekuwa chini ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa tangu mwaka 2006 kutokana na mpango wake wa nyuklia uliopigwa marufuku.

Hatua hizo ziliungwa mkono na Urusi hapo awali, lakini Putin amesema vikwazo hivyo vinapaswa kupitiwa upya.

Putin ameionya pia Korea Kusini kuhusu azma yake ya kuipatia Ukraine silaha, na kusema hilo litakuwa kosa kubwa.