1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kaskazini yazindua manowari ya shambulio la nyuklia

Sylvia Mwehozi
8 Septemba 2023

Korea Kaskazini imetangaza kuwa imeunda manowari ya kimkakati ya shambulio la nyuklia kama sehemu ya juhudi zake za kuimarisha kikosi cha wanamaji.

https://p.dw.com/p/4W5jO
Korea Kaskazini
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na binti yakePicha: KCNA/REUTERS

Korea Kaskazini imetangaza kuwa imeunda manowari ya kimkakati ya shambulio la nyuklia kama sehemu ya juhudi zake za kuimarisha kikosi cha wanamaji. Shirika la habari la serikali la KCNA limeripoti kwamba kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un aliongoza hafla ya uzinduzi huo na kusema kuwa manowari hiyo ni mkakati wa kujiimarisha kiusalama chini ya maji.

Manowari hiyo imepewa nambari 841 na jina la Shujaa Kim Kun Ok. Korea Kaskazini imefanya majaribio kadhaa ya silaha ndani ya mwaka huu huku mwezi uliopita ikishindwa katika jaribio lake la pili la kupeleka satelaiti ya kijasusi kwenye obiti.Korea Kaskazini: Ushirika wa Korea Kusini na Marekani utachochea uhasama

Kwa upande mwingine Korea Kusini na mshirika wake Marekani nazo pia zimeongeza ushirikiano wa kiulinzi kwa kufanya luteka za pamoja za kijeshi.