1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Ushirika wa Korea kusini na Marekani utazidisha uhasama

29 Aprili 2023

Dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya Marekani na Korea Kusini yanayolenga kuimarisha usalama wa Korea Kusini yatazidisha uhasama kwenye rasi ya Korea.

https://p.dw.com/p/4Qhmi
Kim Yo-jong
Picha: Yonhap/picture alliance

Matamshi hayo ya Kim Yo Jong, mwanamke aliye na usemi mkubwa katika utawala wa Korea Kaskazini yanafuatia ahadi ya Marekani ya kuipatia Korea Kusini taarifa zote muhimu na mipango ya Washington ya kuzuia kitisho cha nyuklia cha Korea Kakszaini.

Ahadi hiyo ilitolewa mapema wiki hii wakati wa mkutano kati ya rais Joe Biden wa Marekani na mwenzake wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol mjini Washington.

Soma zaidi:Marekani na Korea Kusini zajadili njia za kukabiliana na kitisho cha mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini

Jong amesema mkataba baina ya Washington na Seoul utaifanya Korea Kaskazini kuimarisha zaidi uwezo wake wa kuzuia kutokea vita vya nyuklia.

Yumkini matamshi yake yanaaminisha Pyongyang haitasitisha majaribio yake ya silaha nzito amabyo yamekuwa yakikosolewa na jirani yake pamoja na Marekani,