1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kaskazini yarusha kombora la masafa marefu Japan

16 Machi 2023

Korea Kaskazini imerusha angalau kombora moja la masafa marefu kuelekea Bahari ya Japan, saa chache kabla ya ziara ya Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol mjini Tokyo.

https://p.dw.com/p/4OkoX
Südkoreas Präsident Yoon Suk-yeol
Picha: Daewoung Kim/REUTERS

Seoul imesema jeshi lake liligundua kombora lililorushwa kutoka eneo la Sunan huko Pyongyang.

Wizara ya Ulinzi ya Japan imethibitisha tukio hilo, ikisema kombora hilo lilikadiriwa kuanguka nje ya eneo la Japan, takriban kilomita 550 mashariki mwa rasi ya Korea.

Walinzi wa pwani wa Japan wamezitaka meli zinazosafiri katika eneo hilo kuwa makini kutokana na mabaki yanayoweza kuelea baharini.

Ni tukio la tatu la kudhihirisha uwezo wa Korea Kaskazini tangu siku ya Jumapili, wakati wiki hii Korea Kusini na Marekani zikiendelea na mazoezi yao makubwa zaidi ya kijeshi katika miaka mitano, luteka zinazochukuliwa na Pyongyang kuwa ni za kivamizi na uchokozi.