1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kaskazini yarejesha shughuli za kijeshi mpaka na Seoul

27 Novemba 2023

Korea Kusini imesema, Korea Kaskazini inarudisha tena vituo vyake vya ulinzi katika eneo la mpaka baina ya nchi hizo mbili ambako ilikuwa imeviondowa kufuatia makubaliano yaliyofikiwa huko nyuma kati ya nchi hizo.

https://p.dw.com/p/4ZTtX
Südkorea-Nordkorea Spannungen
Mpaka kati ya Korea mbili.Picha: Ahn Young-joon/AP Photo/picture alliance

Wiki iliyopita Korea Kusini ilisema itayasitisha kwa muda makubaliano na jirani yake Kaskazini na kuanza tena operesheni ya kufuatilia matukio kwenye eneo la mpaka kufuatia kitendo hicho cha Korea Kaskazini.

Korea Kusini imeitaja hatua yake hiyo kama mipango ya kujilinda kufuatia hatua iliyochukuliwa na jirani yake.

Soma pia: Marekani na Korea Kusini zarekebisha makubaliano ya kuikabili Korea Kaskazini

Wizara ya  ulinzi ya Korea Kusini pia imesambaza kwenye vyombo vya habari picha  inazosema  zinaonesha shughuli za kijeshi katika eneo la mpaka upande wa Kaskazini.

Rais Yoon Suk Yeol ametoa amri, jeshi  la nchi hiyo lifuatilia kwa karibu kinachoendelea na kujiweka katika hali ya tahadhari.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW