1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kaskazini yakanusha kubadilishana silaha na Urusi

17 Mei 2024

Korea Kaskazini imekanusha na kutupilia mbali madai ya Marekani na Korea Kusini kwamba ilibadilishana silaha na Urusi.

https://p.dw.com/p/4fxth
Kim Yo Jong
Dada wa kiongozi wa Korea Kusini Kim Yo JongPicha: Jorge Silva/AP Photo/picture alliance

Korea Kaskazini imekanusha na kutupilia mbali madai ya Marekani na Korea Kusini kwamba ilibadilishana silaha na Urusi. Hayo yameelezwa na Kim Yo Jong dada wa Kiongozi wa taifa hilo ambaye amesema tuhuma hizo ni za uzushi na upuuzi na kwamba silaha za Pyongyang ni kwa ajili ya ulinzi wake.

Hapo jana, Marekani iliwawekea vikwazo watu na makampuni kadhaa ya Urusi kwa kuwezesha usafirishaji wa silaha kati ya Urusi na Korea Kaskazini, ikiwa ni pamoja na makombora ya masafa marefu yanayotumiwa na Moscow nchini Ukraine.

Uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Urusi umeimarika kufuatia ziara ya  Kim Jong Un nchini Urusi mnamo mwezi Septemba mwaka jana, ambapo alikutana kwa mazungumzo na mwenyeji wake Rais Vladimir Putin na kuahidi kuimarisha mahusiano yao ya kijeshi.