1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yafyetua makombora mapya

27 Machi 2023

Korea Kaskazini imefyatua leo asubuhi makombora mawili ya masafa mafupi kuelekea pwani ya Bahari yake ya Mashariki.

https://p.dw.com/p/4PIE4
Nordkorea | Test einer Unterwasserdronhe
Picha: Yonhap/picture alliance

Hilo ni tukio la hivi karibuni kabisa katika msururu wa ufyatuaji makombora kufuatia luteka za kijeshi zinazoendelea kati ya Marekani na Korea Kusini.

Jeshi la Korea Kusini limelaani vikali harakati hizo na kusema ni uchochezi mkubwa unaokiuka maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuitaka Pyongyang kusitisha mara moja vitendo hivyo.

Serikali ya Japan pia imepinga vikali hatua hiyo ya Korea Kaskazini, ikisema kurushwa kwa makombora hayo kunatishia si tu usalama na amani wa Japan, bali pia wa kanda nzima na hata Jumuiya ya kimataifa.

Korea Kaskazini imesema itaendelea na majaribio mengine ikiwa Marekani na Korea Kusini hawatositisha luteka yao ya kijeshi.