1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea kaskazini na Iran zatakiwa kuachana na mipango yao ya Kinuklea.

15 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF3U

Vienna:

Shirika la Umoja wa mataifa la nguvu za Atomiki, limeitaka Korea kaskazini kufuta kabisa mpango wake wa silaha za kinuklea, na kuishauri pia Iran kuuhakikishia Ulimwengu kwamba nayo haifuati mfano wa Korea kaskazini. Nchi hizo mbili zilizotajwa na Rais George W. Bush wa Marekani kuwa “Mhimili wa maovu“, ni miongoni mwa mada muhimu zinazojadiliwa mnamo wiki hii na halmashauri ya magavana wa Shirika hilo la Umoja wa mataifa mjini Vienna , ukiwa ni mkutano wao wa robo ya pili ya mwaka . Wakati Korea kaskazini imedai ina silaha za Kinuklea , Iran imesisitiza kwamba mpango wake ni wa amani, ikiwa tu na lengo la kuongeza kiwango chake cha nishati.