1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKorea Kaskazini

Korea Kaskazini: Luteka ya kijeshi ya Marekani imevuka mpaka

2 Februari 2023

Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini imesema luteka ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na washirika wake imevuka mpaka na kuifanya hali kuwa ngumu zaidi.

https://p.dw.com/p/4N0Qf
Nordkorea Kim Jong Un
Picha: Korean Central News Agency/Korea News Service/AP/picture alliance

Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini imesema luteka ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na washirika wakeimevuka mpaka na kuifanya hali kuwa ngumu zaidi.

Taarifa iliyotolewa leo na wizara hiyo imeeleza kuwa hali hiyo inatishia kuigeuza Rasi ya Korea kuwa ghala kubwa la silaha na eneo muhimu zaidi la kivita, kwa sababu Marekani inafuata sera za uhasama.

Tangazo hilo linatolewa kujibu matamshi ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, ambaye wakati wa ziara yake mjini Seoul siku ya Jumanne, alisema nchi yake itaongeza upelekaji wa silaha na vifaa vya kijeshi katika Rasi ya Korea, ikiwemo ndege za kivita, huku ikiimarisha mafunzo ya pamoja na Korea Kusini.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Korea Kaskazini itajibu shughuli zozote za kijeshi zitakazofanywa na Marekani, na ina mkakati madhubuti wa kukabiliana nazo.