1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Korea Kaskazini kuacha kutuma maputo ya taka Korea Kaskazini

3 Juni 2024

Korea Kaskazini imesema itaacha kutuma maputo yaliyojaa takataka nchini Korea Kusini.

https://p.dw.com/p/4gYfk
Südkorea Müllballons aus Nordkorea
Picha: Im Sun-suk/Yonhap/AP/picture alliance

PyongYang imesema imechukua hatua hiyo ya kutotuma tena maputo hayo kwasababu Korea Kusini sasa imefahamu vya kutosha jinsi inavyohisi.

Tangazo hilo limetolewa masaa machach baada ya Korea Kusini kusema kwamba hivi karibuni itaiadhibu hiyo nchi jirani yake kwa hatua ambazo haitoweza "kuzihimili" kutokana na vitendo vyake hivyo vya kurusha maputo na vitendo vingine vya uchokozi.

Wachambuzi wanasema huenda Korea Kusini ikaanza kurusha ndani ya taifa la Korea Kaskazini, matangazo ya kuonesha ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo na pia kupeperusha taarifa ya habari za dunia pamoja na kucheza miziki ya mtindo wa pop.

Korea Kaskazini inahofia sana matangazo kama hayo kwa kuwa sehemu kubwa ya idadi ya watu wake milioni 26 wako gizani katika habari za ulimwengu, kwani hawapati kutazama rasmi televisheni za kimataifa na kusikiliza vipindi vya redio.