1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongamano la Kimataifa la Vyombo vya Habari laanza leo Bonn

17 Juni 2024

Kongamano la Kimataifa la Vyombo vya Habari linaloandaliwa na Deutsche Welle (GMF) limeanza leo mjini Bonn likikutanisha waandishi na wadau wa habari takriban 1,500 kutoka zaidi ya mataifa 100.

https://p.dw.com/p/4hA7W
GMF 2024 | Washiki wakiwa ndaniya Kongamano
Washiriki Kongamano la Kimataifa la Vyombo vya Habari GMF 2024Picha: Philipp Böll/DW

Akizungumza katika kongamano hilo waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema sio jambo la kukubalika kwa waandishi habari kuuwawa wakiwa kazini kama inavyotokea Gaza. 

Maudhui makuu ya kongamano hilo linalofanyika leo na kesho hapa bonn, ni kusaka masuluhisho katikati ya changamoto na vitisho kadha wa kadha vinavyoletwa na teknolojia ya akili mnemba, ambako waziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani ametoa tamko juu ya hilo na kusema AI ni kitisho na fursa kwa ulimwengu wa habari na demokrasia. 

Soma pia:GMF: Kuchangiana Masuluhisho dunia inapokabiliwa na migogo

Mengine yatakayojadiliwa ni usalama wa wadau wa vyombo vya habari kisaikolojia kimwili kisheria na kiuchumi. Kwa sababu pia mwaka huu wa 2024 ni mwaka ulio na chaguzi nyingi kuanzia  India Umoja wa Ulaya na Marekani, namna ya kuripoti chaguzi mbali mbali pia ni jambo litakalokuwepo mezani kujadiliwa.