1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la Dunia liandaliwe kila baada ya miaka miwili?

20 Desemba 2021

FIFA inaandaa mkutano wa kilele wa kimataifa kwa njia ya video kuujadili mradi wa kuandaa mashindano ya Kombe la Dunia kila baada ya miaka miwili badala ya mzunguko wa sasa wa miaka minne.

https://p.dw.com/p/44a4g
Österreich Wien | Gianni Infantino, FIFA-Präsident
Picha: Joe Klamar/AFP/Getty Images

Mradi wenye utata wa FIFA wa kuandaa Kombe la Dunia kila baada ya miaka miwili badala ya mzunguko wa sasa wa miaka minne umerudi tena mezani huku shirikisho hilo la kandanda ulimwenguni likiandaa leo mkutano wa kilele wa kimataifa kwa njia ya video na mashirikisho yake 211 wanachama.

Hakutakuwa na kura itakayopigwa lakini rai swa FIFA Gianni Infantino amesema wazo ni kutafuta muafaka.

Je, mashirikisho ya kitaifa yanataka kweli kuwa na mashindano ya mara kwa mara ya Kombe la Dunia, au mpango huo unaopigiwa upatu na Arsene Wenger utasambaratika?

Kuna wanaokosoa wakisema mpango huo utakuwa na madhara kwa afya ya wachezaji kutokana na mrundiko wa mashindano. Wenger anahoji kuwa wachezaji wengi hawapati fursa nyingi za kujiendeleza lakini nchi 133 hazijawahi kushiriki katika Kombe la Dunia. FIFA inasema mpango huo utatengeneza faida Zaidi na kusambaza Afrika, Asia na Amerika Kusini.

afp, reuters, dpa, ap