1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KOMBE LA CHALLENGE JUMAMOSI HII LAELEKEA WAPI: ETHIOPIA AU BURUNDI ?

23 Desemba 2004
https://p.dw.com/p/CHZg

FINALI YA CHALLENGE CUP:ETHIOPIA YAUMANA NA BURUNDI (JUMAMOSI HII)

Je, Burundi itaweza kugeuka jogoo la shamba linalowika mjini ? Linabidi kufanya hivyo leo ikiwa lataka kuipiku Rwanda na kutwaa Kombe hilo kwa mara ya ksanza.

Katika changamoto za nusu-finali juzi jumatano mjini Addis, Burundi iliisangaza Sudan kwa kuizaba mabao 2:1 na hivyo imeingia kwa mara ya kwanza finali ya Kombe hili la Challenge.

Ethiopia ilitoka suluhu mabao 2:2 na Harambee Stars-Kenya,lakini katika mikwaju ya penalty kuamua mshindi,Ethiopia iliitoa Kenya kwa mabao 5-4.Kenya iliania ijumaa nafasi ya tatu katika changamoto na Sudan

Waethiopia walitoa Kenya kwa mabao 2-1 ili kutwaa Kombe nchini Rwanda,miaka 3 iliopita,walitia mabao yao yote ya mikwaju ya penalty.Kenya ikicheza na wachezaji 10 tu uwanjani jana, iliwaona wenyeji Ethiopia wakitangulia kwa mabao 2:0,lakini harambee Stars wakidai kutangulia si kufika,walifufuka katika kipindi cha pili pale Mike Muiruri na John Baraza kila mmoja alipotia bao na kusawazisha.

Hatima ya Kenya lakini iliamuliwa katika zahama ya mikwaju ya penalty.Alikua mlinzi wa Harambee Stars Pascal Ochieng alieshindwa kutia bao pale m kwaju wake ulipita juu ya lango la Ethiopia.

Waburndi wamemsangaza kila mmoja katika mashindano haya na wamepiga hatua kubwa zaidi hata kuliko majirani zao rwanda, walioshiriki mapema mwaka huu katika changamoto ya Kombe la Afrika la mataifa huko Tunisia.

Waburundi wanacheza keshokutwa jumamosi finali yao ya kwanza ya Kombe la Challenge Cup na mjini Bujumbura,endapo wakirudi na Kombe mwishoni mwa wiki hii,itakua asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu atie gongo-mkutano uwanja wa ndege.,

Ugandan Cranes-timu ya Taifa ya Uganda,ndio mabingwa wa kwanza wa Kombe hili 1973 .

Uganda wakati ule waliishinda Tanzania mabao 2:1 kutwaa ubingwa na ni Waganda pia walioitoa Rwanda mabao 2:0 kutawazwa mwaka jana mabingwa wa Kombe hili.Jumamosi hii ,mabingwa wapya watatawazwa kitini mjini Addis na ikiwa kweli mcheza kwao hutunzwa,Waethiopia hawataliacha Kombe la challenge Cup 2004 kuondoka Addis.waburundi watakuwa na ajenda nyengine.

Wakati Kenya Harambee Stars, imepiga hatua hadi nusu-finali na kutimuliwa nje kwa bahati mbaya ya mikwaju ya penalty,timu 2 za Tanzania,ziliaga mashindano na mapema.Tanzania-bara hasa ilifanya vibaya na ndio ilioburura mkia katika kundi lake lililojumuisha Rwanda,Ethiopia,Zanzibar na Burundi.Kushiriki kwa Tanzania-bara katika kinyan’ganyiro hiki kulikua mashakani na imekwenda addis bila ya hata viongozi waliosalia nyumbani kuania madaraka katika uchaguzi wa keshokutwa jumatatu mjini Dar-es-salaam.

Mashabiki wengi wa michezo Tanzania,wamevunjwa moyo na mabishano yasiokwisha katika uongozi wa chama chao cha mpira na kurejea nyuma kwa dimba na michezo mengine Tanzania.Jumatatu hii chama cha mpira cha tanzania-bra kinafanya uchaguzi wake kumaliza mgogoro wa uongozi na pengine kufunfua ukurasa mpya katika dimba la Tanzania.

Wiki hii,FIFA-shirikisho la dimba ulimwenguni lilimtawaza kitini ‘MWANASOKA WAKE WA MWAKA WA DUNIA".Chipukizi stadi wa Brazil,Ronaldinho aliwapiku washambulizi hatari-mfaransa Thiery Henry na Muukrain,mwanasoka wa mwaka wa Ulaya-Andriy Shevchenko wa Ukrain na kutawazwa mwanadimba wa mwaka wa FIFA.Kwanini kura ilim,uangukia Ronaldinho licha ya kwamba mpira unaamuliwa kwa mabao na yeye hakutia magoli mengi kama Thiery Henry au Shevchenko walivyotia?

Klabu ya Ronaldinho-FC Barcelona anakocheza pamoja na mchezaji bora wa dimba wa mwaka wa afrika 2003 –Mkameroun,Samuel Eto’o,inaelekea shukurani kwa mabao ya Ronaldinho na Eto’o kutwaa ubingwa wa spain msimu huu,kwani Barcelona wiki hii tu imetawazwa mabingwa wa nusu-msimu.

Isitoshe, Brazil,timu ya Taifa ya Ronaldinho iko njiani kutoroka na tiketi yake ya kushiriki katika Kombe lijalo la dunia hapa Ujerumani 2006 kutoka kanda ya Amerika ya kaskazini.

Ni mfalme Pele binafsi aliemtangaza Ronaldinho kuwa ‘mchezaji bora kabisa wa dimba katika kombe la dunia 2002 huko Korea kusini na Japan.

Bila ya shaka,Ronaldinho alikua ufunguo wa taji la 5 la ubingwa wa dunia pale Brazil ilipoizaba Ujerumani mabao 2:0.Pamoja na wenzake Ronaldo na rivaldo,Ronaldinho ni ‘R’ watatu katika safu ya Brazil,ulimuacha nje Roberto Carlos.

Pasiozake maridadi, mikwaju yake ya freekick ya ajabu na jinsi anavyolisarifu dimba, ni kilele cha msimu ingawa wa kuvunja moyo wa klabu yake ya hapo kabla ya Ulaya Paris St.Germian alikocheza bega kwa bega na stadi mwengine wa Afrika-J.J.Okocha.

Chini ya kocha kutoka Holland, Frank Rijkaard, Ronaldinho,amejiwinda msimu huu kumpiku Ronaldo na Roberto carlos na kuitawaza Barcelona mabingwa wapya wa Spain.Si ajabu kuwa hata manchester united wakati mmoja ilimtaka Ronaldionho katika safu yao,kwani waingereza wanakumbuka vyema mkwaju wake wa free-kick katika kombe la dunia uliozima vishindo vya Uingereza mbele ya Brazil na kumfanya kipa wao Seaman,kuduwaa.

Kocha mashuhuri wa Bayern Munich hadi msimu uliopita,Ottmar Hitzfeld,amearifu kwamba huenda akazingatia kurejea uwanjani kama kocha mwishoni mwa msimu huu-hii ni baada ya kukataa maombi ya kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Ujerumani na hata la Real Madrid ya Spain.Hitzfeld alieiongoza tangu borussia Dortmund hata Bayern Munich kutwa Kombe la klabu bingwa la Ulaya-champions League, amesema hatachukua jukumu lolote hadi Julai mosi, mwakani.