1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kocha wa Augsburg kukosa mechi na Wolfsburg

Deo Kaji Makomba
15 Mei 2020

Nchini Ujerumani Kocha mkuu wa timu ya soka ya Augsburg Heiko Herrlich atakosa mechi yake ya kwanza kutokana na kukiuka sheria za kukaa karantini kabla ya kuanza tena kwa Bundesliga.

https://p.dw.com/p/3cJQ2
Heiko Herrlich wird Trainer des FC Augsburg
Picha: picture-alliance/SvenSimon/F. Hoermann

Ijumaa (15.05.2020) wachezaji wa Augsburg walikuwa wakifanya mazoezi bila kocha Herrlich baada ya kukubali kukiuka sheria kali ya kuwekewa karantini ambayo imemuweka nje kuelekea mechi ya kuanza tena kwa Bundesliga dhidi ya Wolfsburg, baada ya ligi hiyo kusimamishwa kwa muda ikiwa ni juhudi za kuepusha uwezekano wa kuenea kwa maambukizi mapya ya virusi vya Corona.

Herrlich, aliteuliwa siku tatu tu kabla ya ligi kusimamishwa katikati ya mwezi Machi kufuatia mripuko wa janga la virusi vya Corona, aliuambia mkutano wa waandishi wa habari Alhamisi tarehe 14.05.2020 kwamba aliondoka hotelini ambapo timu yake imepiga kambi kwenda kununua dawa ya meno na mafuta maalumu ya ngozi.

Lakini kutokana na hatua madhubuti za kuwekwa karantini kwa timu zote kuelekea kuanza tena kwa Bundesliga, kuingia kwake ndani ya duka hata akiwa amevaa barakoa inamaanisha yeye atakosa mchezo wake wa kwanza Jumamosi na hawawezi kurudi kufundisha timu hadi pale atakapopima mara mbili virusi vya homa ya Sars-CoV-2 na kukutikana hana maambukizi.

1. Bundesliga | Eintracht Frankfurt - FC Augsburg
Picha: picture-alliance/J. Ferreira

Jarida la Kicker katika wavuti yake lilizungumzia juu ya lengo lake zuri, nalo gazeti la Bild lilisema ni ajabu kuwa kocha wa watu wote, ambaye ni mfano wa kuigwa, amekiuka sheria.

Alhamisi (14.05.2020) Herrlich aliomba radhi katika taarifa iliyotolewa kupitia kilabu yake, akisema kuwa hatasimamia timu hata kabla ya bodi ya ligi ya soka ya Ujerumani, (DFL) ingekuwa na uwezekano wa kuweka vikwazo sawa.

"Nilifanya makosa kuondoka katika hoteli hiyo. Hata ingawa niliona hatua za usafi hotelini na hivyo, siwezi kutengua hatua hii. Katika hali hii, sikufanya kama mfano wa kuigwa kwangu, timu na umma," alisema.

"Kwa hivyo nitafanya kwa uadilifu na nikubali kosa langu. Kwa sababu ya mwenendo wangu mbaya, sitajihusisha katika mazoezi ya timu kesho, wala sitaongoza timu dhidi ya Wolfsburg Jumamosi."

Kosa la Herrlich lilikuwa ukiukwaji wa hivi karibuni wa usafi madhubuti itifaki iliyoundwa na DFL ambayo iliruhusu kupata idhini kutoka viongozi wa serikali kuanza msimu tena wa Bundesliga bila ya kuwa na mashabiki uwanjani.

DFL bado haijatoa maoni juu ya tukio hilo lakini imekuwa na hafla kadhaa kuhimiza kila mtu kufuata kabisa itifaki kuepukana na aina yoyote ya kurudisha nyuma.

"Ni kwa kiwango cha juu zaidi cha nidhamu na uangalifu tunaweza kufikia lengo letu la kawaida, msimu wa mwisho 2019/20, "ilielezwa katika mwongozo wake wa kuanza upya kwa Bundesliga.

Wachezaji waadhibiwa

Katika wiki zilizopita, mshambuliaji wa Hertha Berlin, Salomon Kalou, alituma video kwenye mitandao ya kijamii inayoonyesha ukiukaji wa wazi wa kusogeleana na watu na alisimamishwa haraka na kilabu hiyo.

Mchezaji Amine Harit wa Schalke na mlinzi wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani, Jerome Boateng, kutoka kwa mabingwa wa Bundeliga, Bayern Munich, walilipiwa faini na vilabu vyao baada ya kukiuka sheria kali za kukaa karantini nchini Ujerumani.

Tukio la hivi karibuni linaweza kuzusha hisia za wale ambao wanapinga kuanza tena kwa Bundesliga, na tafiti mbili zilizochapishwa Ijumaa zikisema idadi kubwa ya Wajerumani hawataki wachezaji wa mpira kucheza tena msimu huu.

"Deutschlandtrend" ilisema kwamba asilimia 56 ya hao waliopiga kura hawakubaliani na kuanza tena kwa Bundesliga, na asilimia 31 tu ndio wanaopendelea kuanza tena kwa kitimtimu cha ligi hiyo.

Na Deo Kaji Makomba/ap