1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund na VfL Bochum mubashara DW Kiswahili Jumamosi hii

29 Agosti 2023

Ligi kuu kandanda ya Ujerumani, Bundesliga, inaendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali wikendi katika mechi za mzunguko wa pili.

https://p.dw.com/p/4VajO
Bundesliga Grafiken Spieltag 2 | Bochum vs Dortmund HAU
Mechi ya Borussia Dortmund na Bochum itakuwa mubashara kupitia idhaa ya kiswahili ya DW

Ligi kuu kandanda ya Ujerumani, Bundesliga, inaendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali wikiendi katika mechi za mzunguko wa pili. 

Vijana wa Edin Terzic, Borussia Dortmund, wataifuata VFL Bochum katika uwanja wa Vonovia Ruhrstadion.

Bochum walichezea magoli 5 kwa 0 dhidi ya VFB Stuttgart katika mchezo wa ufunguzi wa ligi.

Dortmund kwa upande wao waliwachakaza FC Cologne goli 1 kwa bila.

Mechi hii itatangazwa mubasharana na DW Kiswahili katika mtandao wa Facebook na kupitia redio washirika kuanzia saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika ya Mashariki..

Fußball Bundesliga | Werder Bremen vs Bayern München | Tor  Harry Kane
Mshambuliaji mpya wa Bayern Munich, Harry Kane.Picha: Christof Kopesel/Getty Images

FC Cologne watakuwa nyumbani hapo kesho kukipiga dhidi ya Wolfsburg nyumbani RheinEnergie Stadion.

FC Cologne ilipoteza mchezo wa awali dhidi ya Dortmund lakini Wolfsburg walianza kwa kishindo kwa kuidungua Heidenheim magoli 2 kwa mtungi. 

Siku ya Jumapili, mabingwa wa mara 11 mfululizo wa Bundesliga, Bayern Munich, watakuwa nyumbani Allianz Arena kuwakaribisha Augsburg.

Katika mechi ya ufunguzi Bayern Munich walianza kwa kishindo kwa kuisambaratisha Werder Bremen nyumbani magoli 4 kwa bila.

Nyota mpya wa Bayern Munich anatarajiwa kuendelea kuonyesha makeke yake kwenye klabu yake mpya ya Thomas Tuchel.

Huu ni msimu wa 61 wa Bundesliga na hii ni raundi ya pili ya msimu wa mpya ligi hiyo ya Shirikisho la Ujerumani kwa mwaka 2023/2024.