1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KITISHO CHA SILAHA KILIVUMBULIWA

29 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFo6

LONDON: Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair upya anashinikizwa kukiri kuwa alikosea kuhusu suala la silaha za maangamizi za Iraq.Hali hiyo mpya imezuka baada ya mkuu wa kiraia wa Kimarekani nchini Iraq,Paul Bremer kutamka kinyume na madai ya Blair kuwa kumepatikana ushahidi mkubwa wa miradi ya Saddam Hussein kuhusika na silaha za maaangamizi.Bremer katika mahojiano na stesheni ya televisheni ya ITV alipoulizwa ikiwa ni kweli ushahidi umepatikana kama alivyotamka Blair,alijibu hajui maneno hayo yametokea wapi.Waziri wa kigeni wa zamani wa Uingereza Robin Cook aliejizulu kwa sababu ya serikali ya Uingereza kuamua kwenda vitani dhidi ya Iraq,amesema si jambo la heshima kwa waziri mkuu kuendelea kuamini kitisho ambacho kila mmoja huona kuwa kitisho hicho kilivumbuliwa.Hilo ni jambo linalolitia taifa wasi wasi.Akaongezea kusema kuwa imani ikipotea ni vigumu sana kuirejesha,na hali hiyo imewafanya raia kuwa na shida kuiamini serikali.Cook akakanusha pia kuwa opresheni iliyoongozwa na Marekani nchini Iraq inaweza kuelezwa kama ni ushindi.