Kisa cha mwanajeshi kuuawa chaibua maandamano Chad
6 Septemba 2023Muuguzi wa kijeshi katika kambi ya Ufaransa iliyoko kaskazini mwa Chad amemuua kwa risasi mwanajeshi wa Chad aliyemshambulia, hatua iliyoibua maandamano ya wakaazi wa eneo hilo.10 wauawa katika mapigano nchini Chad
Gavana wa jimbo la Borkou Jenerali Ali Maide Kebir ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kisa hicho kilitokea jana Jumanne katika kambi ya Faya-Largeau, ambako wanajeshi hupelekwa chini ya mkakati wa Ufaransa wa kupambana na wanamgambo ya jihadi nchini humo.
Gavana huyo amesema mwanajeshi huyo aliyekuwa amejeruhiwa na kwenda kambini hapo kwa ajili ya kufungwa kidonda alimshambulia muuguzi huyo kwa kutumia kisu cha upasuaji na kumjeruhi muuguzi huyo, hatua iliyomfanya muuguzi kujihami kwa kumfyatulia risasi.Balozi wa Marekani awasili Chad kukutana na wakimbizi wa Sudan
Taarifa za kifo hicho zilizusha maandamano ya siku nzima ya wakazi wa Faya nje ya lango kuu la kambi hiyo na kujaribu kuingia ndani ingawa hawakufanikiwa, amesema Maide Kebir.