1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kipindupindu chaanza baada ya mafuriko Msumbiji

1 Aprili 2019

Mji wa Beira ulioharibiwa na kimbunga cha Idai nchini Msumbiji, umethibitisha kifo cha kwanza kutokana na mripuko wa kipindupindu, huku visa vya ugonjwa huo vikipanda hadi 517.

https://p.dw.com/p/3G2T5
Mosambik, Beira: WHO bereitet Cholera-Impfungen in Mosambik vor
Picha: picture-alliance/dpa/T. Mukwazhi

Vituo vya afya vya dharura vimeundwa ili kudhibiti mripuko huo katika mji wa Beira wenye wakaazi 500,000, amesema mkurugenzi wa idara ya afya ya taifa ya Msumbiji Ussen Isse, kulingana na kituo cha Televisheni ya Taifa; TVM.

Visa vya kipundupindu kibaya vimeongezka pakubwa tangu visa vitano vya kwanza viliporipotiwa wiki ilyopita.

Kimbunga Idai kiliharibu vibaya mfumo wa maji wa mji wa Beira kilipoushambulia Machi 14.

KAribu chanjo 900,000 za Kipindupindu zinatarajiwa kuwasili hii leo kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO.