1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

kiongozi wa zamani wa chama cha kikomunisti,Zhao Ziyang afariki

17 Januari 2005

Aliyekuwa kiongozi wa chama cha kikomunisti nchini china Zhao Ziyang amefariki hii leo alfajiri.Ziyang amefariki akiwa na miaka 85 baada yakuugua ugonjwa wa kiarusi.

https://p.dw.com/p/CHhl

Aliyekuwa kiongozi wa chama cha kikomunisti nchini china Zhao Ziyang amefariki hii leo alfajiri.Ziyang amefariki akiwa na miaka 85 baada yakuugua ugonjwa wa kiarusi.

Hadi kifo chake kiongozi huyo alikuwa amefungiwa nyumbani kufuatia kuunga mkono maandamano ya kutaka mageuzi huko Tiananmen katika mwaka wa 1989.

Kiongozi huyo wa zamani wa chama cha kikomunisti hakuwahi tena kuiona nje kwa jicho lake kwa zaidi ya miaka 15, hadi kifo chake hii leo, kufuatia na madai ya kuunga mkono maandamano ya mwaka 1989 huko Tiananmen uchina.

Zhao Ziyang amefariki dunia hii leo asubuhi kufuatia kuugua kwa muda ugonjwa wa kiarusi ambapo alikuwa amelazwa kuanzia siku ya ijumaa akiwa katika hali ya coma katika hospitali ya Beijing hii leo alfajiri.

Hali ya usalama imeimarishwa katika siku za hivi karibuni kwenye eneo la Tiananmen kutokana na hofu kwamba huenda kifo cha bwana huyo kikazua vurumai jingine jipya la watu wanaounga mkono mageuzi ya kisiasa nchini humo.

Kifo cha Zhao Ziyang kimezua hisia kali miongoni mwa watu wa china ikiwa ni pamoja na aliyekuwa katibu wake, Bao Tong ambaye ametumikia kifungo cha miaka saba na sasa anaishi chini ya ulinzi wa serikali, ametoa taarifa ya kuishutumu vikali serikali ya China kwa kumfungia Zhao nyumbani kwa zaidi ya miaka 15 , huku akisema kuwa ni kitendo cha udhalilifu alichofanyiwa marhum Zhao na pia cha kutia aibu kwa watetezi wa haki nchini humo pamoja na chama cha kikomunisti.

Kufuatia kifo cha Zhao Ziyang, waziri mkuu wa china bwana Junichiro Koizumi ameitolea wito serikali yake kufanya juhudi za kuleta demokrasi.Hata hivyo wachunguzi nao pamoja na wanaharakati wa kisiasa wanasema juhudi za bwana Zhao za kuleta mageuzi ya kisiasa nchini humo hazikuwa na uzito katika kizazi ambacho tayari kimejitolea kupigania mageuzi hayo.

Kulingana na mwanafunzi mmoja kutoka chuo kikuu cha Carliforinia,Richard Baum anasema hivi sasa kwa mtu wa kawaida nchini china hakuna anayehisi uchungu wowote kutokana na kifo cha Zhao na hii ni kutokana na kutotambulika kwake na raia wa kawaida.

Zhao aliweza kutambulika kama mtu mwenye usemi mkubwa nchini China .kutokana na hilo basi,akafungiwa ndani kwa kupinga uamuzi wa aliyekuwa chifu mkuu wakati huo Deng Xiaoping wakutaka kuwamaliza wandamanaji kwa kutumia matanki.

katika uhai wake Zhao,wapinzani wake na wale waliomrithi madaraka walihofia huenda akaunganisha watetezi wa mageuzi,wafanyikazi waliokuwa wananung’unikia ongezeko la watu wasio na ajira,na wakulima waliokuwa wakihisi kuna pengo kubwa nchini humo baina ya maskini na matajiri.

Lakini chama cha kikomunisti chini ya Hu na Wen kimeungana kikiwa na mwelekeo wa kufikia lengo la kuwepo mageuzi na kukifanya kuwa wazi bila ya kuhatarisha uwezo wa kuhodhi mamlaka yake.Ijapokuwa upande mwingine walihisi kwamba China ingali changa mno kuwepo demokrasi.

Mkewe Liang Boqi ambaye alikuwa naye katika vita dhidi ya Japan yupo katika hali mbaya ya kiafya.Zhao amewaacha nyuma watoto wanne wakiume na mmoja wakike na wajukuu wanne.

Mkewe Liang Boqi ambaye alikuwa naye katika vita dhidi ya Japan yupo katika hali mbaya ya kiafya.Zhao amewaacha watoto wanne wakiume na mmoja wakike na wajukuu wanne.