1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Kiongozi wa Taiwan asema China haina haki ya ´kuwaandama´

24 Juni 2024

Rais wa Taiwan Lai Ching-te amesema kuwa China haina haki ya kuwaadhibu watu wa Taiwan kutokana na maoni yao au harakati zao.

https://p.dw.com/p/4hQmy
Rais wa Taiwan Lai Ching-te
Rais wa Taiwan Lai Ching-te.Picha: Sam Yeh/AFP

Hii ni baada ya Beijing kuwaonya wale iliowaita wafuasi sugu wanaounga mkono uhuru wa kisiwa hicho kwamba huenda wakakumbwa na adhabu ya kifo.

Lai amesema kuwa demokrasia sio chanzo cha uhalifu bali utawala wa kibabe ndio uhalifu.

Kiongozi huyo ameonya kuwa mahusiano kati ya pande hizo yataendelea kuzorota ikiwa China haitaitambua Jamhuri ya China, ambalo ndilo jina rasmi la Taiwan na kufanya mazungumzo na serikali halali ya Taiwan iliyochaguliwa kidemokrasia.

China inadai kuwa Taiwan ni sehemu ya himaya yake na imekataa kufuta uwezekano wa kutumia nguvu ili kuchukua udhibiti wa kisiwa hicho.