1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa JEM ameuawa na Jeshi la Sudan

Gakuba,Daniel/zpr26 Desemba 2011

Jeshi la Sudan limearifu kuwa limemuua kiongozi wa kundi la waasi la Justice and Equality Movement -JEM- Khalil Ibrahim, alipokuwa akijaribu kuingia kwa siri katika Sudan Kusini.

https://p.dw.com/p/13ZEM
Kiongozi wa kundi la JEM, Dr.Khalil Ibrahim ameuawa

Msemaji wa jeshi la Sudan, Al-Sawarmi Khalid ameiambia televisheni ya taifa kuwa kamanda huyo wa JEM na makamanda kadhaa wa JEM waliuawa katika mapigano makali yaliyotokea.

Kwa upande mwingine, JEM lakini imekanusha habari za kutokea mapigano hayo. Kundi hilo limesema, kamanda wao na mlinzi wake waliuawa katika mashambulizi ya ndege Ijumaa iliyopita na kuongezea kuwa kufanikiwa kwa shambulio hilo lililomlenga Khalil Ibrahim, hudhihirisha kuwa kulikuwepo njama za usaliti kutoka ndani na nje ya kanda hiyo.

Wachambuzi wanakichukulia kifo cha Khalil Ibrahim kama ni pigo kubwa kwa kundi la JEM ambalo ni kundi kubwa kabisa katika jimbo lenye machafuko Darfur, magharibi ya Sudan.