1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEthiopia

Kiongozi wa chama cha Ezema nchini Ethiopa akamatwa

27 Septemba 2023

Kiongozi wa chama cha upinzani kinachotetea haki za raia nchini Ethiopia (Ezema) Chane Kebede, amekamatwa mjini Adis Ababa na nyumba pamoja na ofisi yake kupekuliwa. Chama chake kimeeleza Jumanne (27.09.2023)

https://p.dw.com/p/4Wr90
Äthiopien EZEMA-Parteikampagne in Bahr Dar
Viongozi wa chama cha EZEMA wakifanya kampeini katika eneo la Bahr DarPicha: Alemenew Mekonnen/DW

Seyoum ameliambia shirika la habari la AFP kwamba hawajui kwa nini Chane alikamatwa na kwamba kuna uvumi  huenda hatua hiyo inahusiana na ghasia na hali ya sasa ya hatari katika eneo la Amhara. Seyoum amesema kukamatwa kwa Chane hakukuzingatia utaratibu wa kikatiba na kwamba alichukuliwa na watu wasiojulikana kwenye gari lisilo na namba za usajili.

Chane bado hajashtakiwa mahakamani

Seyoum ameongeza kuwa Chane bado yuko kizuizini katika kituo cha uchunguzi wa uhalifu mjini Addis Ababa, zaidi ya saa 48 baada ya kukamatwa, lakini bado hajahojiwa au kufikishwa mahakamani. Serikali ya shirikisho ilikuwa imetangaza mnamo Agosti 9 kwamba wapiganaji wa kundi la wanamgambo walikuwa wamejiondoa kutoka miji mikubwa ya Amhara, lakini ghasia zinaendelea katika maeneo kadhaa.

Soma pia:Mgogoro wa Ethiopia watishia uthabiti wa kikanda-UN

Mapema mwezi Agosti, serikali ya waziri mkuu Abiy Ahmed, ilitangaza hali ya hatari katika jimbo la Amhara baada ya mapigano kuzuka kati ya vikosi vya serikali na kundi moja la wanamgambo linalojulikana kama Fano.

Hatua hiyo inaipa mamlaka nguvu za kuwakamata watu, kuweka sheria za kutotoka nje na kupiga marufuku mikusanyiko ya hadhara. Shirika la kutetea haki za binadamu la Ethiopia, limeshutumu vikosi vya serikali kwa kutekeleza mauaji ya kiholela huko Amhara pamoja na kuwaweka kiholela watu wengi kizuizini chini ya hali hiyo ya hatari.

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed akiwa mjini Roma nchini Italia mnamo Februari 6, 2023
Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy AhmedPicha: Massimo Percossi/Ansa/ZUMA Press/IMAGO

TPLF yataka kuongezwa kwa muda wa Tume ya Kimataifa ya Wataalamu wa Haki za Kibinadamu kuhusu Ethiopia (ICHREE)

Wakati huo huo, vyombo vya habari nchini Ethiopia vimeripoti kuwa chama cha Ukombozi wa watu wa Tigray, TPLF kinataka kuongezwa kwa muda wa kuhudumu kwa Tume ya Kimataifa ya Wataalamu wa Haki za Kibinadamu kuhusu Ethiopia (ICHREE) inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa huku kukiwa na ripoti za kuendelea kwa ukiukaji wa haki licha ya mkataba wa kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka miwili katika eneo la kaskazini mwa Tigray.

Soma pia:Amnesty International yavituhumu vikosi vya Eritrea kufanya ukatili Tigray

Vyombo hivyo vimeendelea kuripoti kuwa kundi la TPLF limesema kuongezwa kwa muda huo, kutaiwezesha tume hiyo kutimiza wajibu wake ipasavyo na kutekeleza mkataba wa amani wa Pretoria na serikali ya shirikisho.

Ripoti moja iliyochapishwa na ICHREE mnamo Septemba 18, ilisema kwamba hali katika eneo la Tigray bado ni mbaya huku ukatili, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu vikiendelea kufanyika nchini humo na amani bado haijapatikana.

Soma pia:Wanajeshi wa Ethiopia wanawarudisha nyuma wapiganaji wa Amhara

Katika hatua nyingine, Jeshi la Ukombozi la Oromo (OLA-Shene) limesema linaunda kikosi chake cha jeshi ambacho Waoromia wanastahili lakini bado hakijaanza kujihusisha kikamilifu katika shughuli za kijeshi baada ya kukwama kwa mazungumzo ya amani kati yake na serikali mnamo mwezi Mei.