1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTunisia

Kiongozi maarufu wa upinzani Tunisia akamatwa

24 Februari 2023

Vikosi vya usalama nchini Tunisia vimemkamata kiongozi mashuhuri wa upinzani Jawhar Ben Mbarek, ikiwa ni ukamataji wa hivi karibuni zaidi katika msako dhidi ya wapinzani wa Rais Kais Saied.

https://p.dw.com/p/4Nwvm
Tunesien Tunis | Proteste gegen Präsident Kais Saied
Picha: Hassene Dridi/AP/picture alliance

Wakili wake amesema Ben Mbarek ambaye ni mwanachama wa ngazi za juu wa muungano wa upinzani wa National Salvation Front FSN, na kiongozi wa vuguvugu linaloitwa "raia dhidi ya mapinduzi" alikamatwa jana usiku na hadi sasa hajafunguliwa mashtaka yoyote.

Ben Mbarek ambae ni mbobezi wa masuala ya sheria kama alivyo Rais Kais, alimuunga mkono katika jitihada zake za urais mwaka 2019, lakini tangu wakati huo amekuwa ni mkusoaji mkubwa wa serikali iliyoko madarakani.

Tunisia imeshuhudia wimbi la kamatakamata la viongozi wa kisiasa na wakosoaji wa rais, huku tukio la hivi karibuni zaidi likiwa ni siku ya Jumatano ambapo polisi ilimkamata mwanasiasa mkongwe Chaima Issa.