1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bazoum ataka mahakama ya kikanda itoe amri ya kuachiwa kwake

21 Septemba 2023

Kiongozi aliyepinduliwa Niger Mohammed Bazoum amefungua shauri la kuitaka mahakama ya Jumuiya ya ECOWAS itoe amri kwa majenerali wanaomshikilia kumwachia huru na kumrejesha madarakani.

https://p.dw.com/p/4Wd6p
Nigers Präsident Bazoum in Paris | Archivbild
Picha: Stevens Tomas/ABACA/IMAGO

Kwenye maombi yaliyowasilishwa mahakamani wiki hii, Bazoum anataka Jumuiya hiyo ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS itangaze kuwa uamuzi wa wanajeshi kumweka kizuizini, unakiuka haki zake za msingi na kwamba yeye bado ni kiongozi halali wa Niger. 

Bazoum aliondolewa madarakani katika mapinduzi ya Julai 26 na tangu wakati huo, yeye pamoja na familia yake wanashikiliwa na wanajeshi waliochukua madaraka.

Macron asema balozi wake nchini Niger anaishi kama mateka

LichNiger yaituhumu Ufaransa kutaka kuishambuliaa ya shinikizo la kimataifa, majenerali waliompindua wamekataa miito ya kumwachia huru au kumrejesha madarakani na wao kuachia hatamu za kuliongoza taifa hilo.