1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron asema balozi wake nchini Niger anaishi kama mateka

Sylvia Mwehozi
16 Septemba 2023

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema balozi wake nchini Niger na wafanyakazi wengine wanaishi kama mateka ndani ya ubalozi wa nchi hiyo mjini Niamey.

https://p.dw.com/p/4WPWW
Indien I G20 - Emmanuel Macron
Picha: Arif Hudaverdi Yaman/AA/picture alliance

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema balozi wake nchini Niger na wafanyakazi wengine wanaishi kama mateka ndani ya ubalozi wa nchi hiyo mjini Niamey. Macron amewashutumu watawala wa kijeshi kwa kuzuia kupelekwa chakula ndani ya ubalozi huo. Ameeleza kwamba afisa huyo hawezi kutoka nje baada ya kuondolewa kinga ya kidiplomasia na amekataliwa kupewa chakula.

Maandamano ya kutaka wanajeshi wa Ufaransa waondoke yafanyika NigerMaandamano ya kutaka wanajeshi wa Ufaransa waondoke yafanyika NigerViongozi wa kijeshi wa Niger walitoa saa 48 kwa balozi wa Ufaransa nchini humo Sylvain Itte kuondoka mara moja, wakati walipomwondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum Julai 26. Lakini balozi huyo hakuondoka ndani ya muda huo uliotolewa huku serikali ya Ufaransa ikigoma kutambua utawala wa kijeshi.

Ufaransa inao wanajeshi wapatao 1,500 nchini Niger, na ilisema mapema mwezi huu kwamba kupelekwa tena kwa wanajeshi kunaweza tu kujadiliwa na Bazoum.