1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Waasi wa FDLR waishutumu Rwanda

9 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEcx

Waasi wakihutu wanaoendesha shughuli zao katika nchi ya kidemokrasi ya Kongo wameshutumu serikali ya kigali kwa kupanga hujuma dhidi ya uchaguzi wa Kongo.

Msemaji wa waasi wa chama cha FDLR Anstase Munyandekwe ameliambia shirika la habari la AFP kwamba serikali ya Kigali haitaki kuiona kongo ikielekea kwenye demokrasi.

Ameongeza kusema kwamba Rwanda inataka kuzuia kupatikana demkrasia Kongo ili iweze kuiba mali ya nchi hiyo.

Zoezi la uadikishaji wapiga kura nchini Kongo unaendelea wakati uchaguzi ukitarajiwa kufanyika Juni mwaka 2006.

Huo utakuwa ni uchaguzi wa kwanza utakaofanyika kwa njia ya kidemokrasi katika kipindi cha miaka 40.