1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Askari polisi zaidi kuongezwa na Umoja wa Mataifa,Kongo.

7 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEdY

Umoja wa Mataifa ambao kwa sasa una kikosi kikubwa cha kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kuliko sehemu yoyote duniani,unakusudia kuongeza askari polisi wengine 841 nchini humo,chini ya muswada uliopitishwa na Baraza la Usalama la Umoja huo jana.

Maofisa hao wa polisi watakaoongezwa wanakusudiwa kufanya kazi ya kuwafunza askari polisi wa Kongo,kuzuia vitendo vyovyote vya ghasia kutoka kwa raia na pia kusimamia mchakato wa kuelekea uchaguzi wa kidemokrasia.

Watu milioni 30 nchini Kongo wanatazamiwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu,ambao bado tarehe kamili ya kufanyika haijatangazwa,lakini unatakiwa lazima ufanyike kabla ya tarehe 30 mwezi wa Juni mwakani.