1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Watu wenye silaha waliowateka nyara wafanyakazi wa Medecins Sans Frontieres wawaacha huru.

11 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF4d

Katika jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, watu wenye silaha wamewaacha huru wafanyakazi wawili wa shirika la kutoa huduma ya afya la madaktari wasio na mipaka waliowateka nyara.

Msemaji wa shirika hilo mjini Geneva amethibitisha kuachwa huru kwa wafanyakazi hao , ambao ni raia mmoja wa Ufaransa na dereva wake raia wa Congo. Watu hao walitekwa nyara wakiwa njiani kuelekea katika kambi ya wakimbizi katika jimbo la Ituri wiki iliyopita.

Shirika la madaktari wasi na mipaka Medecins Sans Frontieres limesema kuwa watu hao wako katika hali nzuri kiafya.

Mapigano ya kikabila katika jimbo hilo lenye mzozo, karibu na mpaka na Uganda, yamesababisha kiasi cha watu 60,000 kupoteza maisha na kulazimisha watu zaidi ya 500,000 kuyahama makaazi yao katika muda wa miaka sita iliyopita.