1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA : Watu wenye silaha bado wako Kinshasa

2 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDFs

Mjumbe mwandamizi wa Ulaya kwa Afrika ya Kati amesema hapo jana bado kuna watu wengi wenye silaha katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Kinshasa ikiwa ni siku 10 baada ya makundi hasimu ya kisiasa kupambana katikati ya mji mkuu huo na kusababisha kuuwawa kwa watu 23.

Wanajeshi watiifu kwa Rais Joseph Kabila na wale wa hasimu wake Makamo wa Rais Jean-Piere Bemba viongozo ambao watapambana katika marudio ya uchaguzi wa Urais hapo mwezi wa Oktoba wamekuwa wakionekana ndani ya mji huo mkuu licha ya makubaliano ya tarehe 22 Augusti kutaka waondoke kwenye mji huo.

Mwakilishi huyo maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Nchi za Maziwa Makuu barani Afrika Aldo Ajello ameliambia shirika la habari la AFP mwishoni mwa safari yake ya siku saba kwenye mji mkuu wa Congo kusaidia kutuliza mvutano kwamba kuna watu wengi wenye silaha wanazunguka katika mji wa Kinshasa.