1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Wanyarwanda kutatizana Kongo na UN

20 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFhd

Ofisi ya jeshi la Umoja wa Mataifa Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imelaumu makamanda wa jeshi la waasi wa Rwanda kwa kuwazuwia askari wao na familia zao kusafirishwa kurudi nyumbani. Afisa wa jeshi la MONUC mjini Kinshasa amesema kuwa makamanda hao walipanga vizuwizi vya kijeshi barabarani kuwazuwia wanajeshi wao wapatao elfu 3 na familia zao, baada ya kuomba Umoja wa Mataifa msaada wa kuwarejesha Rwanda wakitokea kambi moja ya mkoa wa Kivu kaskazini. Imedaiwa pia na afisa huyo kuwa wanamgambo hao wa kinyarwanda wamerusha pia risasi dhidi ya maafisa wa Umoja wa Mataifa waliojaribu kuwasiliana na baadhi ya wanajeshi waliokuwa wameomba kusafirishwa kurudi Rwanda.