1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Wanamgambo wanyangánywa silaha kwa nguvu

2 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFQz

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo,hii leo imeanza kwa nguvu kuwanyangánya silaha wanamgambo katika eneo la Ituri kaskazini-magharibi mwa nchi.Opresheni hiyo imeanzishwa siku moja baada ya kumalizika ule muda uliotolewa kwa wanamgambo kutoa silaha zao kwa hiyari.Opresheni ya tume ya Umoja wa Mataifa,MONUC ilianzishwa asubuhi ya leo katika maeneo ya Bolonzabo,kilomita 12 kusini-magharibi ya Bunia-mji mkubwa katika jimbo la Ituri na pia katika eneo la jirani la Kodeza.Kwa makadirio ya MONUC kuna kiasi ya wanamgambo 200 katika sehemu hizo.Hadi siku ya Ijumaa takriban wapiganaji 6,600 wa zamani walitoa silaha zao katika eneo la Ituri,kabla ya kumalizika muda waliopewa kufanya hivyo.