1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Waasi wa LRA kusakwa nchini JK ya Kongo.

6 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEUd

Umoja wa Mataifa umepeleka mamia kadhaa ya askari kwenye sehemu ya ndani ya J. K. ya Kongo ili kuwakabili waasi wa Uganda Lord Resistance Army.

Kuwapo kwa waasi hao nchini J. K. ya Kongo kumesababisha mzozo wa kidiplomasia baina ya nchi hiyo na Uganda.

Mapema wiki jana Uganda ilitishia kupeleka wanajeshi wake ndani ya Kongo ili kuwafuatilia waasi hao, lakini Kongo imesema hatua hiyo ingehatarisha amani.

.