1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Umoja wa Mataifa wakanusha askari wake kuhusika na mauaji Kongo.

4 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFZr

Msemaji wa Umoja wa Mataifa katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amekanusha madai ya kuwa majeshi ya Umoja huo yamewauwa raia katika jimbo la Ituri kaskazini mashariki mwa Kongo.

Mashambuliano ya risasi yalizuka baina ya watu waliojihami kwa silaha wa kabila la Lendu na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa katika kambi karibu na mji wa Bunya katika jimbo la Ituri siku tano baada ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa tisa kuuwawa mahali hapo.

Umoja wa Mataifa ulisema kuwa wapiganaji wa kikabila 50 waliuwawa na wanajeshi wawili wa Umoja wa Mataifa wakajeruhiwa.

Mapema kiongozi wa kabila la Lendu alisema raia 25 wakiwemo wanawake na watoto waliuwawa.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan amesema kuwa hali ya Kongo huenda ikahitaji wanajeshi zaidi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.